Deuteronomy 9:26-28

26 aNilimwomba Bwana na kusema, “Ee Bwana Mwenyezi, usiangamize watu wako, urithi wako mwenyewe ule ulioukomboa kwa uweza wako mkuu na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu. 27 bWakumbuke watumishi wako Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Usiangalie ukaidi wa watu hawa, uovu wao wala dhambi yao. 28 cWatu wa nchi ile uliyotutoa sisi wasije wakasema, ‘Ni kwa sababu Bwana hakuweza kuwachukua mpaka nchi aliyokuwa amewaahidia, kwa sababu aliwachukia, akawaleta ili aje kuwaua jangwani.’
Copyright information for SwhKC